Sunday, July 1, 2012

ULIMBOKA NA POLISI WANA MASWALI YA KUJIBU

Najaribu kujiuliza maswali mengi ili nipate kuamini kama ni serikali imehusika kumdhuru dr Ulimboka kama ambavyo wengi wanaamini lakini bado naishia 50/50

Hii ni kwa ukweli kwamba timing ya tukio inanifanya nihusishe na mgomo lakini jinsi tukio lenyewe lilivyofanyika linanipa maswali makubwa sana.

Yapo maswali ambayo ulimboka inabidi ayajibu lakini pia yapo maswali ambayo TISS inabidi ijiulize

Kwa mujibu wa ulimboka, alipigiwa simu na MTU ANAYEFANYA KAZI IKULU kwa kujitambulisha kwa muda wa siku 3 mfululizo, hapa yanaibuka maswali matatu

1. Kama serikali imehusika moja kwa moja, kwa nini ijitambulishe vile, hapa kuna swali, kwa nini aliyepiga simu aseme anafanya kazi ikulu, ina maana ikulu ilitaka kumteka ulimboka lakini sio kwa siri, kila mtu ajue ni ikulu imefanya hivyo?

2. Lakini pia ulimboka anasema huyu mtu kampigia simu kwa muda wa siku 3, kweli TISS inafanya kazi kizembe hivi haiwezi kumpata ulimboka mpaka wampigie simu aje mwenyewe? Hawajui kazini anatoka saa ngapi? Na JE kumpigia simu siku 3 zote hawakuhofia kuwa Ulimboka anaweza shtuka au akaja eneo wanalomwita tayari kashajipanga na watu wake??

3. Kama alipigiwa simu siku 3 mfululizo, polisi waanzie hapa kufanya kazi, nadhani itakuwa ni line mpya lakini kwa ninavyojua mimi, simu ukinadilisha line, kule kwenye mtambo wanaweZa kwambia simu ile ilikua inatumia namba gani kabla, na ile namba ilikuwa inawasiliana na nani!

Swali jengine linalonitia mashaka ni kwamba Dr ulimboka anasema pale leaders club alienda na dokta mwenzie ila kutekwa alitekwa yeye tu, JE huyu dokta alikuwa wapi baada ya tukio, JE ALITOA TAARIFA KITUO CHOCHOTE CHA POLISI? Manake kutekwa ni tukio kubwa na wanakiri kuwa walishaanza kuwa na wasiwasi

Dr ulimboka pia anasema watekaji walikua na bunduki kubwa moja ambayo hakuweza itambua, polisi tanzania wanatumia bunduki ya aina moja tu ambayo ukiiona utaijua na kwa kuwa walishaamua kumteka bila kuficha kwa kusema wanatoka ikulu, hawakua na sababu kutafuta bunduki ya aina nyengine ili isitambulike kama ni ya polisi

Maswali ni mengi sana lakini mungu ampe uzima wa haraka ili aje atusaidie tumjue mbaya wetu, yawezekana mtu akaja tumia udhaifu huu, akamdhuru kiongozi mmoja wa upinzani kwa kusema anafanya kazi ikulu halafu amani tutaisikia kama wasomali wanavyoiota

Lakini kama Ulimboka ataamua kukaa kimya na kutowataja "watesi" wake, basi ipo hatari Mtanzania mwengine kutekwa na kuteswa kwa style ile ile aliyotekwa Ulimboka na kuifanya Tanzania si salama