Siku za karibuni kuna miswada
mitatu imepitishwa bungeni kwa hati ya dharura na kuleta taharuki ya kuwa ''nchi
inauzwa', Serikali imeleta miswada mibovu, mafuta yetu na gesi zetu mafisadi
wachache wanataka kunufaika peke yao na kelele nyingi sana.
Swali linalonijia, kwa nini
''hati ya dharura''? na kwa nini wapinzani wasusuie, na wafanye vurugu mswada
usijadiliwe? kwa maoni yangu kuna mambo mawili matatu yamejitokeza.
Kwanza pengine huu mswada una maslahi binafsi na wanaoupitisha ndio manahawajatupa muda wa kuujadili, au Mheshimiwa Rais
anataka akumbukwe kuwa yeye ndio aliyeleta mapinduzi haya yaliyomo kwenye
mswada au haamini atakayemuachia kiti cha Urais kama atakubali mswada huu
upitishwe kama ilivyokuwa kwa awamu zilizopita.
Lakini pia naamini kamwe
Wapinzani wasingekubali kukaa chini kukubali kuujadili ule mswada na kuupitisha
kwa sababu ndani ya mswada ule kuna majibu ya mambo mengi ambayo Wapinzani
wanasema CCM wamefeli na wao wakiingia madarakani watafanya.
Kwa sababu serikali haikutaka
kushirikisha wananchi, walichokifanya wapinzani kimeonekana ni kitendo cha
kishujaa na uzalendo wa hali ya juu.
Najua wengi hamjapata muda wa
kusoma Mswada wa Mafuta na Gesi, vifuatavyo ni baadhi ya vipengele vya mswada
huo nimevikopi bila kuongeza neno ili muangalie kama mswada ni mzuri au mbaya
na kwa nini uharaka wenye mashaka.
8.-(1) Tanzania Petroleum Development Corporation
shall be the National Oil Company and shall, in that respect, undertake Tanzania’s commercial aspects of petroleum in the
upstream, midstream and downstream operations and participating interests of
the Government in the petroleum and natural gas agreements.
(3) The licence granted to the National Oil Company shall not be transferable to any other person.
(b)details of exemptions, variations or suspensions of conditions of licence and permit;
(2) Where goods and services required by the
contactor or licence holder are not available in Tanzania, such goods shall be
provided by a company which has entered into a joint venture with a local
company.
hivyo ni vipengele vichachache kati ya vipengele vipi vya mswada huu. kama unataka kuusoma utaupata kwa urahisi kwenye blog ya john mnyika kwa anuani ya mnyika.blogspot.com