Monday, July 15, 2013

Wito wa kusitisha tozo/kodi ya laini ya simu kufuatia mabadiliko ya sheria ya kodi 2013


WITO WA KUSITISHA TOZO/KODI YA LAINI YA SIMU KUFUATIA MABADILIKO YA SHERIA YA KODI 2013

CHANGE TANZANIA timu! Wakati ni kwetu kuonyesha kuwa mabadiliko ni sisi na si kusubiri mtu mwingine alete mabadiliko. Tembelea tovuti hii (http://www.avaaz.org/en/petition/WITO_WA_KUSITISHA_TOZOKODI_YA_LAINI_YA_SIMU_KILA_MWEZI_KUFUATIA_MABADILIKO_YA_SHERIA_YA_KODI_2013/?copy  na uweke sahihi yako kupitia mtandao ili kuikataa kodi au tozo kandamizi ya  laini ya  simu (Sim card tax). Tusaidiane tukusanye sahihi milioni moja ili tuweze kuiwasilisha bungeni mwezi wa nane . Ni dakika chache tu toa muda wako muhimu kulijenga Taifa lako, watanzania tumekuwa na utamaduni wa muda mrefu wa kulalamikia vitu na kuvihacha viendelee japo atukubaliani navyo, kwa kusaini hapo kwenye link kwa pamoja tutakuwa na sauti moja katika ili, pia itasaidia kumtetea mwananchi wa hali ya chini ambaye ndo anaumizwa sana  na kodi au tozo hii kandamizi kila mwezi, serikali inaweza bana matumizi ili kutekeleza bajeti yake, pia kuna vyanzo vingine vya kodi kama tulivyoelezea kwenye hiyo petition. Shawishi na wenzako angalau 100 waweze saini zao pia, kwa kadri tunakavyoweza pata idadi kubwa ndivyo tutakavyopata uwezo wa kusimamisha hii kodi, nchi ni wananchi, sisi ni wananchi.
   Mabadiliko kwa vitendo.