Wapo wengi walioajiriwa wanatamani kuanzisha mradi huku wakiendelea kuwa kazini, na kwa kuwa hawawezi kuacha kazi wanaishia kununua bodaboda, bajaj, au taxi... At the end of the day wanaishia kugombana na madereva
Guys mradi wowote unahitaji capital na muda wa ufatiliaji la sivyo utatwanga maji kwenye kinu
Kama capital unayo fungua duka food staffs, kama mtaji wako mzuri zaidi waweza fungua mini supermarket, lakini sio uswahilini coz biashara za huko ni Za maduta ya taa na sembe huwezi icontrol ukiwa kazini
Waweza pia anzisha biashara ya diesel kama una capital ya @least 15000$, inalipa vizuri kama laki mbili kwa siku wakati biashara inaanza, ukichangamka inalipa vizuri saaaaaaana
Nnavyosikia sikia uwakala wa Mpesa na Tigo pesa pia unalipa pia. 5mil Capital can make difference
Biashara ya kununua gari japan kwa kulipia online then ikija hapa utauza au kununua ili uuze na wewe upo kazini full time itakula kwako
Ushawahi fikiria biashara ya packaging? Kwa mfano unasajili jina, then unakuwa na brand yako ya sukari ya mfuko wa kilo moja unasupply kwenye supermarkets... Capital ya 7mil inatosha
Salon za kike na za kiume pia sinalipa bt sijawahi fanya hio biashara
Wale ndugu zangu wa mbeya wanajua ule mpango wa kununua mchele wakati wa msimu na kuuza wakati wa kiangazi.. Inalipa pia kama hutaki chakarika saaana..
Zipo biashara nyingi kwa wenye capital, kana capital yako ndogo, acha kazi ukuze mtaji.. Nitafunguka zaidi nikipata muda
Thursday, June 14, 2012
Tuesday, June 5, 2012
TUMETOA DODOKI, TUMEWEKA JIWE LA KUSUGULIA MIGUU
Wakati wa bunge la budget mwaka 2011, mheshimiwa kafulila alimtuhumu Bw Zambi na mbunge mwenzie Omary badwel kwa kuomba rushwa wanapoenda kufanya kazi, akaamriwa kukaa chini
Mheshimiwa felix mkosamali akasimama kuomba muongozo wa mwenyekiti wa bunge ambaye alikuwa mh Simbachawene kwa kuwa tuhuma ni nzito kwa mbunge kuambiwa kaomba rushwa mbele ya bunge tukufu
Mh Simbachawene akasema atalitolea maelezo lakini mpaka leo akalipotezea na hakusema chochote
Leo hii, badwel, mwaka mmoja baadae anakamatwa kwa kosa lile lile la kuomba Rushwa na kufikishwa mahakamani na bw Simbachawene leo hii kapandishwa na kuwa naibu waziri wa nishati na madini.. Usishangae siku akipewa uwaziri kamili wizara hiyo. Wizara yenye kashfa za kutosha..

Monday, June 4, 2012
KATIBA NIITAKAYO
1. SYSTEM OF ELECTION IBADILIKE
hapa Tanzania tumezoa first past the post FPTP ambayo anayeongoza kwa kura anachukua madaraka. kwa mtazamo wangu system hii ya uchaguzi ndiyo inayotufanya tushindwe kupiga kura kwa upande mmoja lakini kwa upande wa pili, inasababisha upotevu wa kura nyingi. kwa mfano Rais Kikwete anaongoza nchi kwa kupata kura 5,276,827 ambayo ukigawanya kwa watanzania miloni 40 ni sawa na aslimia 12.5 ya watanzania wote
lakini pili Dr slaa alipata kura 2,271,941 ambazo ni karibia nusu ya kura Za kikwete, hii ni kusema zaidi ya watu milioni mbili maoni yao hayajasikilizwa. haiwezekekani watanzania zaidi ya milioni mbili wamchague mtu halafu maoni yao yapotee kwa kuwa wamezidiwa na wengine, kesho hawatapiga kura
katiba mpya ilete system ya propotional Representative ambayo uwakilishi serikalini utatokana na idadi ya asilimia katika kura zilizopigwa. Kwa system hii, hakuna kura itakayopotea kwa maana, hata group dogo la watu kura zao zitapata muwakilishi kwenye serikali hivyo watanzania wataamka kupiga kura
2. MFUMO WA SERIKALI 3
So far tuna mfumo wa serikali mbili, serikali kuu na SMZ, haya ni mapungufu. Zanzibar imeungana na maiti? Tanganyika irudi iwe na serikali yake, Zanzibar iwe na serikali yake na kuwe na serikali kuu ya Tanzania ambayo itakuwa na Rais, makamu, waziri wa ulinzi, mambo ya nje na fedha tu. hii itakata mzizi wa fitina.
3. RAIS ASISHITAKIWE LAKINI, ALIPE MSHAHARA NA POSHO ALIYOPEWA KAMA HAKUTIMIZA AHADI
najua hii itasound kama kichekesho lakini ilani ya uchaguzi ya mgombea husika ni kama business plan, wananchi wanamchagua mgombea flani kutokana na ilani yake, je kama hakutimiza yale aliyosema atafanya, vipi aondoke na mshahara ambao sisi tumempa kwa kazi ambayo hajaifanya.
tumemuona Obama anahaha kuconvince congress lipitishe mambo yaliyo kwenye ilani yake mfano ahadi juu ya bima ya afya, kwa kuwa hiyo ilani ndio iliyompa uongozi
4. JESHI LA WANANCHI NA MAGEREZA YAWE SEHEMU YA KIJAMII NA 25% YA BUDGET YAKE INJITEGEMEE
tufute leseni zote za wakandarasi kutoka nje na kazi za ujenzi wa barabara na kandarasi kubwa ziende kwa jeshi la wananchi. m not suggesting kuwa jeshi halina kazi, lakini lina human resources nyingi za kuweza kufanya kazi za kandarasi na pesa ya ujenzi ikalipe mishahara. natambua kama JKT wanajitahidi kupitia SUMA JKT lakini JWTZ ndio linaloweza zaidi.
kule south Africa wamepiga marufuku gari za kijapan kutembea kwenye ardhi yao labda kwa kibali maalum tangu walivyoamua kutengeneza magari. tuna jeshi lenye watu shupavu, tuna amani, kwa nini mkandarasi wa barabara ya mwenge ubungo awe mchina????
mwengine kaiba kuku wa 15,000 kafungwa miezi sita katumia chakula cha sh 270'000. kwa nini asiambiwe wewe, na wewe, na wewe, mmehukumiwa kupalilia pamba hii mpaka mavuno
5. SHERIA YA KUMLINDA MLAJI
ukinunua gazeti limeandika habari ya uwongo unaruhusiwa kulishtaki na unalipwa fidia, kampuni ya simu imetangaza shilingi kwa sekunde, ikipandisha bei itangaze au ikikata kinyemela ishitakiwe
6. Waziri asiwe mbunge
7. barabara ikitaka kupita kwenye eneo la makazi ya watu, wasilipwe fidia bali serikali ile gharama stahiki za kununua nyumba eneo lile
8. mwananchi ndio mwenye nchi

Saturday, June 2, 2012
Friday, June 1, 2012
PRICELESS MEMORIES
nilipoamka asubuhi daaaaaah baridi sana na mama ananilazimisha kuoga. nikaoga chap chap, nikavaa bukta yangu ya blue, shati jeupe, kidumu na ufagio mkono wa kushoto, nishapakwa mafuta ya AYUU chap chap.. kwa kuwa kipindi kile sikuwa na saa so sikujua kama nimewahi au nimechelewa shule, kutoka nje watoto wenzangu nao wapo njiani kwenda shule.
mara tukapita sehemu yenye redio, haa kumbe ndio kwanza kipindi cha majira kinaanza, hii itakuwa saa 12 na nusu, tukaanza kucheza njiani, tunaenda shule huku "tunabaka' panzi. kufika shule tumewahi, bbada ya kuhesabiwa namba mstarini wanafunzi wakaambiwa wakafagie, sisi darasa la kwanza tukaanza kucheza makida makida. tunaimba *makiiida makiiiiida makida nzeeee* yeeeeee
ah muda wa darasani si ukafika. tukaanza soma hiiii ndio oooooo, o,o,o, ipo kama yaaaaai o,o,o,oooo. na hii ndio uuuuuuu, u u uu, ipo kama kikoooombeeee u,u,u. kwa kipindi kile sikujua how fun it was leo ndio naona raha yake.
hivi ni shule yetu tu au na nyie mlikuwa mnasema ELOMENO PIIII KYU mkifikia zile alphabets za L M N O P Q ?? hivi ni dunia nzima? na hii W mlikuwa "mnasema double U" mbona imekaa kama "double V"
anyways kengele ikagongwa tulishangiliajeeeeee. kutoka nje najiuliza, hii sh 5 ya kutumia niliyopewa ninunue gudi gudi, au nikanunue mihogo? ah bora nile ashkirimu kwa bibi kibo anauza ashkirimu za maziwa.
sisi tuliotoka shule saa tano tulikuwa na raha, kaka huko darasani kwao ndio kwanza wanasoma kitabu cha darasa la tano, naskia wanasoma "siku ya gulio Katerero" ile ya jana chopeko na mnofu au hadithi ya juma na rosa kama sikosei watakuwa washamaliza kuisoma
basi sisi tukaondoka kulelekea nyumbani huku tunacheza kitenesi ayyyyaaaa mvua ikaanza kunyesha, raha ilioje, nikavua viatu nikaweka kwenye begi nikaaza safari na mvua, meno ya juu yanagonga ya chini kwa baridi, kufika njia ya kanisani, lile kanisa lina paa kuuuuuubwa hivyo maji ya mvua yanatiririka kwa wingi, tukajitega chini ya paa, daaah hiyo mvua inavyotuangukia sasa. barrrriiiidddiiiiiiiii
nyumbani sasa, mama ananiambia baridi inatia homa so nikachange chap chap, nikala kiporo cha ubwabwa na maharage huyoooooo nikaenda angua maembe kwa mzee juma. kumbe kaka angu wana safari ya kishule kutembelea makumbusho ya taifa, wakapita pale nyumbani kwenye gari wamejaaa na walimu wao wanaimba kwa sauti kubwaaa "dereeeeva tubwageeee, dereeeva ongeza mwendoooooo" wana raha, na mimi nikiwa darasa la tano nitaimba kwenye gari
any ways jioni hii mama kanikataza kuwinda ndege, so navaa manati yangu shingoni narudi nyumbani taratiiiiibu huku navizia jirani naona usiku wanapika ubwabwa. hakuna kitu homework na sina haja ya kuwahi kulala leo kwa kuwa kesho ni jumamosi, jambo la muhimu kesho ni kipindi cha mama na mwana muendelezo wa hadithi ya binti chaupele na msimulizi HALIMA KIHEMBA
ah yamepita hayo, mimi leo hii ni waziri, rais, mbunge, muajiriwa, mtu mzima, mheshimiwa na nimewasahau wale wote nilioimba nao ukuti, na nafasi yangu niliyonayo sasa imenitia upofu kabisa juu ya watoto na haki zao, viwanja vyao (open space) tunavidhulumu, walimu hatuwalipi tena mishahara, watoto wa kike ninawatumikisha nyumbani kwangu, watoto wa kiume tumeshawapa ajira ya kuokota vyuma na sina mpango wowote wa kuwasaidia watoto wafurahie utoto wao kama nilivyofurahia mimi... #changeTanzania
#ZANZIBAR REVEALED
kuna dhana ya kuwa karume aliuawa kulinda muungano, mazingira yote ya kuuawa kwa karume haiihusishi tanganyika kwa namna moja ama nyengine katika mauaji hayo na kwamba ni wananchi walichoshwa na serikali yao. kinachotokea leo zanzibar, ni msingi mbovu wa utawala wa tokea awali na kamwe tanganyika isihusishwe.
jarida
moja la kila mwezi 'Africa Events' la Agosti 1992 (uk. 27) ,linadai
sababu za kuuawa kwa Karume zilikuwa za kibinafsi kwa njia ya kulipa
kisasi. Inaelezwa kwamba Muhammed Hamud, mtoto wa Hamud Muhammed Hamud,
aliyetiwa kizuizini miezi michache baada ya mapinduzi ya 1964
akituhumiwa kutaka kuipindua Serikali ya Karume.
Miaka,
rnichache baadaye, Luteni Hamud Muhammed Hamud akiwa katika mafunzo ya
kijeshi huko Tashkent (Urusi ya zamani), aliambiwa na mwanafunzi
mwenzake kwamba mzee Hamud alinyongwa na Karume akiwa kizuizini hila
kufunguliwa mashtaka. Kwa taarifa hiyo, Luteni Hamud alisikika akiapa
angemuua Karume akirejea Zanzibar.
Taarifa
ya kusudio la Hamud la
kuua ilifikishwa kwa vyombo vya usalama Visiwani na wenzake, lakini
hakukamatwa wala kuwekwa wa chini ya uchunguzi mkali aliporejea
Zanzibar; badala yake alipandishwa cheo kuwa luteni na Karume mwenyewe.
Jarida
hili halisemi lolote juu ya raja Ali Khatibu Chwaya na koplo mwingine juu ya kushiriki kwao katika mauaji haya. Hata hivyo,. Kushiriki
kwao kunaelekea kutetea dhana ya pili kwamba kwa sababu Serikali Karume
ilishindwa kukidhi matarajio ya Wazanzibari wengi, hapakuwa na njia
mbadala ila kumwondoa Karume ili kuleta
mabadiliko.
Hapa panazuka swali; kama lengo la Hamud la kumuua Karume lilikuwa kulipa kisasi, kwa nini tukio hili lilihusisha watu zaidi ya mmoja? Si hivyo tu; kwa nini watu zaidi ya 1,000 walikamatwa kutokana na mauaji hayo kama haukuwa mpango mpana?
Dhana
ya kulipiza kisasi inapungua nguvu kwa kushindwa kusimama kwa miguu
miwili. inatuacha njia panda wakati huo ikijaribu kumezwa na dhana
mpango wa mapinduzi, kama ilivyodai Serikali.
Inadaiwa kuwa mpango kuipindua, Serikali ya Karume ulibuniwa mwaka 1968 na wanharakati wa mapinduzi ya 1964 wakiwemo raia na Wanajeshi wachache.
Inasemekana
kikao cha mwisho cha mpango huo kilifanyika Aprili 2, 1972 nyumbani kwa
Luteni Hamud, ambapo ilikubaliwa kwamba mauaji hayo yafanyike Aprili 7,
1972.
Mpango wa utekelezaji ulikuwa kwamba Hamud na Ahmada wachukue jukumu zito sana la kuiba silaha kutoka Kambi ya Jeshi yaBavuai.
Katika kutekeleza mapinduzi hayo, ambayo mipango na operesheni yake ilifanana kabisa na ya mapinduzi ya 1964, mtu mmoja, Suleiman Sisi, alipewa jukumu la kuongoza mashambulizi kwenye Kambi ya Jeshi la Mtoni na Ahmada alipewa jukumu la Kambi ya Bavuai, Makao Makuu ya Jeshi la Chuo cha Jeshi la Mafunzo ya Redio ambazo zote ziko eneo la Migombani.
Kambi ya Ubago haikupangiwa mtekaji kwa kuamini kwamba kama kikosi cha Ahmada kingeweza kuziteka sehemu kilichopangiwa, Ubago ingesalimu amri sawia.
Kituo cha Polisi Malindi kingetekwa na kikosi ambacho kingeongozwa na Hamud, ambapo magari yenye redio za mawasiliano yangepatikana kwa watekaji. Ilipangwa kuwa wakati mashambulizi haya yakiendelea, kituo cha Polisi Ziwani kingevamiwa na askari polisi walitarajiwa kuajiriwa na kuongozwa na askari Yusuf Ramadhan.
Mtu mwingine, Amour Dughesh, alipangwa kuteka Ikulu na alipewa jukumu lakumkamata Karume na kumpeleka Kituo cha Redio kutangaza kupinduliwa kwa Serikali rake.
Inaelezwa pia kwamba baada ya redio kutekwa, ingewekwa chini ya udhibiti wa Badawi Qualletein, Miraji Mpatani na Ali Mtendeni. Uwanja wa Ndege ungedhibitiwa na Ali Sultan Issa, ambapo Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa AS P (ASPYL) yangetekwa na Baramia.
Makao Makuu ya ASPYL yalikuwa Kituo Kikuu cha Mkuu wa Usalama wa Ndani ya Serikali ya Karume, Kanali Seif Bakari. Kanali Bakari aliongoza kikundi cha ukatili kilichojiita kamati ya watu 14, kilichotesa na kuua waliodhaniwa wapinzani na Karume. Abdulrahman Mohammed Babu, akiandikia jarida la kila mwezi 'CHANGE' (Vol 4 No. 7,) la 1996, ukurasa 11, anakiri:- "Kutaja pekee jina la Kamati ya Watu 14 kulitosha kumtia mtu woga na kutishika”.
Kamati hii ilihusika na mauaji ya mamia ya Wazanzibari wasio na hatia, wakiwemo, viongozi, wana’mapinduzi wa kimaendeleo kama Abdallah Kassim Hanga, Abdulaziz Twala, Saleh Saadala, Othman shariff na wengine wale waliuawa kwa jina la Karume."
Abdallah Ameir alipewa jukumu la kuzuia mashambulizi kutoka nje siku hiyo yamapinduzi.
Inadaiwa
kuwa katika kikao hicho, Aprili 2, 1972 mtu mmoja, Amar Salim Kuku,
alidokeza kuwa Ali Salim Hafidh ambaye nafasi yake haikutajwa katika
mpango wa mapinduzi wa Aprili 7, angefika Zanzibar na Abdulrahman Babu
na wafuasi wake wa Dar es salaam, usiku wa Aprili 6 kwa mtumbwi kuungana
na wanamapinduzi wengine.
Ukiwaondoa Luteni Hamud na Kepteni Ahmada katika mpango huu, na kama ni kweli kwamba mpango wote ilikuwa jaribio la mapinduzi (coup d'etat) kama ilivyodai Serikali ya Zanzibar, 'basi staili ya mpango huo haiwezi kutofuatishwa na ile ya mapinduzi ya umwagaji damu ya Aprili 12, 1964 ,ambao haukuhusisha jeshi.
Mapinduzi
ya 1964 ya kushtukizwa dhidi ya utawala wa Sultan Jamshid na majeshi
yake, yalifanikiwa kwa sababu ya utawala huu kujitenga mbali na
wananchi, hivyo haikuweza kupata taarifa za mipango ya mapinduzi hayo
mapema.
Na kama ni kweli ilivyosema Serikali ya Zanzibar, kwamba mpango wa mapinduzi ya 1972 ulibuniwa tangu mwaka 1968, ilikuwaje JWTZ na Usalama wa Taifa, achilia mbali kikosi cha Usalama wa Ndani cha Karume (Gestapo), kilichoongozwa na Kanali Seif Bakari kisibaini mapema hadi siku ya kupoteza uhai wa Kiongozi wa.taifa hilo? Je, si kweli kwamba historia ya 1964 ilikuwa ikijirudia?
Haya yanaweza kuwa maoni ya wengi, wakiwamo wachunguzi wa mambo ya siasa. Mwanazuoni mahiri barani Afrika, Ali Mazrui anabainisha katika kitabu chake 'Africa's International Relations' (uk. 11); "ukizingatia jinsi Sheikh Abeid Karume alivyoitawala Zanzibar kwa ukatili na ubaguzi mkubwa, lolote lilitarajiwa kutokea kwake; hakuna aliyetarajia kwamba angedumu kwa miaka minane madarakani. Ndiyo maana hatimaye wengi hawakushangaa alipouawa mwaka 1972."
Subscribe to:
Posts (Atom)