Friday, June 1, 2012

PRICELESS MEMORIES

nilipoamka asubuhi daaaaaah baridi sana na mama ananilazimisha kuoga. nikaoga chap chap, nikavaa bukta yangu ya blue, shati jeupe, kidumu na  ufagio mkono wa kushoto, nishapakwa mafuta ya AYUU chap chap.. kwa kuwa kipindi kile sikuwa na saa so sikujua kama nimewahi au nimechelewa shule, kutoka nje watoto wenzangu nao wapo njiani kwenda shule.

mara tukapita sehemu yenye redio, haa kumbe ndio kwanza kipindi cha majira kinaanza, hii itakuwa saa 12 na nusu, tukaanza kucheza njiani, tunaenda shule huku "tunabaka' panzi. kufika shule tumewahi, bbada ya kuhesabiwa namba mstarini wanafunzi wakaambiwa wakafagie, sisi darasa la kwanza tukaanza kucheza makida makida. tunaimba *makiiida makiiiiida makida nzeeee* yeeeeee

ah muda wa darasani si ukafika. tukaanza soma hiiii ndio oooooo, o,o,o, ipo kama yaaaaai o,o,o,oooo. na hii ndio uuuuuuu, u u uu, ipo kama kikoooombeeee u,u,u. kwa kipindi kile sikujua how fun it was leo ndio naona raha yake.

hivi ni shule yetu tu au na nyie mlikuwa mnasema ELOMENO PIIII KYU mkifikia zile alphabets za L  M N O P Q ?? hivi ni dunia nzima? na hii W mlikuwa "mnasema double U" mbona imekaa kama "double V"

anyways kengele ikagongwa tulishangiliajeeeeee. kutoka nje najiuliza, hii sh 5 ya kutumia niliyopewa ninunue gudi gudi, au nikanunue mihogo? ah bora nile ashkirimu kwa bibi kibo anauza ashkirimu za maziwa.

sisi tuliotoka shule saa tano tulikuwa na raha, kaka huko darasani kwao ndio kwanza wanasoma kitabu cha darasa la tano, naskia wanasoma "siku ya gulio Katerero" ile ya jana chopeko na mnofu au hadithi ya juma na rosa kama sikosei watakuwa washamaliza kuisoma

basi sisi tukaondoka kulelekea nyumbani huku tunacheza kitenesi ayyyyaaaa mvua ikaanza kunyesha, raha ilioje, nikavua viatu nikaweka kwenye begi nikaaza safari na mvua, meno ya juu yanagonga ya chini kwa baridi, kufika njia ya kanisani, lile kanisa lina paa kuuuuuubwa hivyo maji ya mvua yanatiririka kwa wingi, tukajitega chini ya paa, daaah hiyo mvua inavyotuangukia sasa. barrrriiiidddiiiiiiiii

nyumbani sasa, mama ananiambia baridi inatia homa so nikachange chap chap, nikala kiporo cha ubwabwa na maharage huyoooooo  nikaenda angua maembe kwa mzee juma. kumbe kaka angu wana safari ya kishule kutembelea makumbusho ya taifa, wakapita pale nyumbani kwenye gari wamejaaa na walimu wao wanaimba kwa sauti kubwaaa  "dereeeeva tubwageeee, dereeeva ongeza mwendoooooo" wana raha, na mimi nikiwa darasa la tano nitaimba kwenye gari

any ways jioni hii mama kanikataza kuwinda ndege, so navaa manati yangu shingoni narudi nyumbani taratiiiiibu huku navizia jirani naona usiku wanapika ubwabwa. hakuna kitu homework na  sina haja ya kuwahi kulala leo kwa kuwa kesho ni jumamosi, jambo la muhimu kesho ni kipindi cha mama na mwana muendelezo wa hadithi ya binti chaupele na msimulizi HALIMA KIHEMBA

ah yamepita hayo, mimi leo hii ni waziri, rais, mbunge, muajiriwa, mtu mzima, mheshimiwa na nimewasahau wale wote nilioimba nao ukuti, na nafasi yangu niliyonayo sasa imenitia upofu kabisa juu ya watoto na haki zao, viwanja vyao (open space) tunavidhulumu, walimu hatuwalipi tena mishahara, watoto wa kike ninawatumikisha nyumbani kwangu, watoto wa kiume tumeshawapa ajira ya kuokota vyuma na sina mpango wowote wa kuwasaidia watoto wafurahie utoto wao kama nilivyofurahia mimi... #changeTanzania

5 comments:

  1. Nice article Slim.. Those were the days.. #Memories

    ReplyDelete
  2. hazirudi tena.. siku hizi watoto wanakosa meeengi

    ReplyDelete
  3. evelyn hiyo ndio inabeba story yoooooote ya hapo juu

    ReplyDelete
  4. Utadhani ni mimi nimeitoa hiyo story.. ukitoa part ya manati ... kuangua maembe, kupanda miti ya migazi, kucheza Rede..Ukuti..those days!.. "....hakuna kitu homework na sina haja ya kuwahi kulala leo kwa kuwa kesho ni jumamosi, jambo la muhimu kesho ni kipindi cha mama na mwana muendelezo wa hadithi ya binti chaupele na msimulizi HALIMA KIHEMBA"

    ReplyDelete