Thursday, June 28, 2012
LA ULIMBOKA LIWE FUNZO
Lakini kubwa zaidi lililonitia hamasa ya kuandika ni wepesi wetu watanzania wa kuhukumu, tunawaachia watoto zetu urithi mbaya sana
Nisieleweke kuwa napingana na kile mnachoamini ninyi bali najaribu kwenda zaidi ya imani yenu.
Vipi Mheshimiwa LEMA angefariki kwa kifo cha kawaida tu kama binadamu wengine ambavyo hufa siku ya pili baada ya kumuandikia waraka rais kikwete? Kwa style yetu ya kuhukumu tungekuwa na amani sisi?
Au Vipi kama mimi nakitaka kiti cha mnyika cha Ubunge na hivyo baada ya drama za "rais dhaifu" nikaamua kumvizia na kumdhuru, nani atanihisi? Najua mtakuwa mshamtaja mhusika bila kunihusisha kabisaaa
Naogopa sana kugusia imani ya wengi juu ya kifo cha sokoine na amina chifupa kwa kuwa itanilazimu niamini na kifo cha chacha wangwe
Nilijaribu soma btn the lines chanzo na matukio ya Rwanda genocide na uhusika wa Ufaransa na kagame, halafu nikasoma utawala wa SIAD BARRE wa somalia, utawala wake, kifo chake na somalia ya leo.
Ikulu ni mahali patamu sana, na wanasiasa wana mbinu nyingi sana za kubaki madarakani au kuingia madarakani Ikibidi hata kwa damu, KENYA ni mfano mzuri... TUJIANGALIE TUNAWEZA GONGANISHWA VICHWA KWA USHAHIDI WA KIMAZINGIRA
Lakini swali la msingi, hawa waliomteka dr ulimboka naskia walikua na bunduki, wamezipata wapi? Kama serikali ingeweka ulinzi wa kutosha tusingeihusisha kirahisi katika mambo kama haya, they should play their part or else kila siku tutaihusisha na kila jambo baya
Anyways ni maoni yangu tu ila mtaani kwetu ukimwambia mtu utanikoma wewe siku ya pili akidhurika polisi wanakubeba, zamu yetu sasa na sisi kuamini kama ambavyo wao huamini yale ya mtaani kwetu
Friday, June 22, 2012
MNYIKA HAKUKOSEA
Hivi ni nani hajawahi ona watoto wa darasa la kwanza wanafunga barabara kwa kuwa mwenzao amegongwa mpaka matuta yawekwe, na siku hiyo hiyo matuta yanawekwa? Tumemfundisha nini mtoto huyu? Tumemfundisha serikali yako ni dhaifu lakini ukiishikia kiboko inatekeleza hapo hapo
Wakati wa mkapa wanafunzi udsm waligoma, mkapa akafunga chuo mwaka mzima, hatukusikia tena mgomo mpaka 2007 wakati wa kikwete, tuliposikilizwa tulichogomea, tuligoma kwa kila kitu hata kama hatukustahili
Kitendo cha mtu kusimama mbele ya bunge akapata courage ya kusema rais dhaifu, akarudia na kurudia peke yake inaprove kama rais ni dhaifu
USHAURI WA BURE KWA RAIS:
Haiwezekani sovereign country tunaambiwa kuna muwekezaji ana passport tano, serikali imemshindwa, KWELI? Serikali ya watu mil 40, jeshi, police, na TISS, inaandikwa gazetini imemshindwa mtu mmoja? Vaa mkono wa chuma baba
Hakuna uhuru usio na mipaka mheshimiwa kikwete. He who wishes to be obeyed must know how to command, uhuru ukizidi sana tunaharibu nchi. Unatuachia saaaana mpaka tunaanza kukukosea heshima
Madaktari wamegoma, tukaambiwa rudini kazini haraka au tutawafukuza wote tutaleta wanajeshi wafanye kazi, then kesho tunawaita tunakaa nao mezani, baba watakupanda kichwani washajua una udhaifu, unawaogopa..
Machiavelli anasema If an injury has to be done to a man it should be so severe that his vengeance need not be feared..
Kwa mfano watoto wanagoma lazma matuta yawekwe, waagize walimu wao wawatandike viboko watoto warudi darasani, then baada ya mwezi weka tuta kuzuia ajali kwa kuwa hapo mwanzo walikaa miaka bila tu.
Tunagomagoma kila kitu kwa sababu unaturuhusu, lakini pia haujali.. Wanafunzi wagome, madokta wagome, walimu wagome, hivi nani anawapa kiburi? Hawa madokta nani anawapa kiburi cha kugomea serikali?
Men are so simple and so much inclined to obey immediate needs that a deceiver will never lack victims for his deceptions.
Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network
Thursday, June 14, 2012
Anzisha mradi
Guys mradi wowote unahitaji capital na muda wa ufatiliaji la sivyo utatwanga maji kwenye kinu
Kama capital unayo fungua duka food staffs, kama mtaji wako mzuri zaidi waweza fungua mini supermarket, lakini sio uswahilini coz biashara za huko ni Za maduta ya taa na sembe huwezi icontrol ukiwa kazini
Waweza pia anzisha biashara ya diesel kama una capital ya @least 15000$, inalipa vizuri kama laki mbili kwa siku wakati biashara inaanza, ukichangamka inalipa vizuri saaaaaaana
Nnavyosikia sikia uwakala wa Mpesa na Tigo pesa pia unalipa pia. 5mil Capital can make difference
Biashara ya kununua gari japan kwa kulipia online then ikija hapa utauza au kununua ili uuze na wewe upo kazini full time itakula kwako
Ushawahi fikiria biashara ya packaging? Kwa mfano unasajili jina, then unakuwa na brand yako ya sukari ya mfuko wa kilo moja unasupply kwenye supermarkets... Capital ya 7mil inatosha
Salon za kike na za kiume pia sinalipa bt sijawahi fanya hio biashara
Wale ndugu zangu wa mbeya wanajua ule mpango wa kununua mchele wakati wa msimu na kuuza wakati wa kiangazi.. Inalipa pia kama hutaki chakarika saaana..
Zipo biashara nyingi kwa wenye capital, kana capital yako ndogo, acha kazi ukuze mtaji.. Nitafunguka zaidi nikipata muda
Tuesday, June 5, 2012
TUMETOA DODOKI, TUMEWEKA JIWE LA KUSUGULIA MIGUU
Mheshimiwa felix mkosamali akasimama kuomba muongozo wa mwenyekiti wa bunge ambaye alikuwa mh Simbachawene kwa kuwa tuhuma ni nzito kwa mbunge kuambiwa kaomba rushwa mbele ya bunge tukufu
Mh Simbachawene akasema atalitolea maelezo lakini mpaka leo akalipotezea na hakusema chochote
Leo hii, badwel, mwaka mmoja baadae anakamatwa kwa kosa lile lile la kuomba Rushwa na kufikishwa mahakamani na bw Simbachawene leo hii kapandishwa na kuwa naibu waziri wa nishati na madini.. Usishangae siku akipewa uwaziri kamili wizara hiyo. Wizara yenye kashfa za kutosha..
Monday, June 4, 2012
KATIBA NIITAKAYO
hapa Tanzania tumezoa first past the post FPTP ambayo anayeongoza kwa kura anachukua madaraka. kwa mtazamo wangu system hii ya uchaguzi ndiyo inayotufanya tushindwe kupiga kura kwa upande mmoja lakini kwa upande wa pili, inasababisha upotevu wa kura nyingi. kwa mfano Rais Kikwete anaongoza nchi kwa kupata kura 5,276,827 ambayo ukigawanya kwa watanzania miloni 40 ni sawa na aslimia 12.5 ya watanzania wote
lakini pili Dr slaa alipata kura 2,271,941 ambazo ni karibia nusu ya kura Za kikwete, hii ni kusema zaidi ya watu milioni mbili maoni yao hayajasikilizwa. haiwezekekani watanzania zaidi ya milioni mbili wamchague mtu halafu maoni yao yapotee kwa kuwa wamezidiwa na wengine, kesho hawatapiga kura
katiba mpya ilete system ya propotional Representative ambayo uwakilishi serikalini utatokana na idadi ya asilimia katika kura zilizopigwa. Kwa system hii, hakuna kura itakayopotea kwa maana, hata group dogo la watu kura zao zitapata muwakilishi kwenye serikali hivyo watanzania wataamka kupiga kura
2. MFUMO WA SERIKALI 3
So far tuna mfumo wa serikali mbili, serikali kuu na SMZ, haya ni mapungufu. Zanzibar imeungana na maiti? Tanganyika irudi iwe na serikali yake, Zanzibar iwe na serikali yake na kuwe na serikali kuu ya Tanzania ambayo itakuwa na Rais, makamu, waziri wa ulinzi, mambo ya nje na fedha tu. hii itakata mzizi wa fitina.
3. RAIS ASISHITAKIWE LAKINI, ALIPE MSHAHARA NA POSHO ALIYOPEWA KAMA HAKUTIMIZA AHADI
najua hii itasound kama kichekesho lakini ilani ya uchaguzi ya mgombea husika ni kama business plan, wananchi wanamchagua mgombea flani kutokana na ilani yake, je kama hakutimiza yale aliyosema atafanya, vipi aondoke na mshahara ambao sisi tumempa kwa kazi ambayo hajaifanya.
tumemuona Obama anahaha kuconvince congress lipitishe mambo yaliyo kwenye ilani yake mfano ahadi juu ya bima ya afya, kwa kuwa hiyo ilani ndio iliyompa uongozi
4. JESHI LA WANANCHI NA MAGEREZA YAWE SEHEMU YA KIJAMII NA 25% YA BUDGET YAKE INJITEGEMEE
tufute leseni zote za wakandarasi kutoka nje na kazi za ujenzi wa barabara na kandarasi kubwa ziende kwa jeshi la wananchi. m not suggesting kuwa jeshi halina kazi, lakini lina human resources nyingi za kuweza kufanya kazi za kandarasi na pesa ya ujenzi ikalipe mishahara. natambua kama JKT wanajitahidi kupitia SUMA JKT lakini JWTZ ndio linaloweza zaidi.
kule south Africa wamepiga marufuku gari za kijapan kutembea kwenye ardhi yao labda kwa kibali maalum tangu walivyoamua kutengeneza magari. tuna jeshi lenye watu shupavu, tuna amani, kwa nini mkandarasi wa barabara ya mwenge ubungo awe mchina????
mwengine kaiba kuku wa 15,000 kafungwa miezi sita katumia chakula cha sh 270'000. kwa nini asiambiwe wewe, na wewe, na wewe, mmehukumiwa kupalilia pamba hii mpaka mavuno
5. SHERIA YA KUMLINDA MLAJI
ukinunua gazeti limeandika habari ya uwongo unaruhusiwa kulishtaki na unalipwa fidia, kampuni ya simu imetangaza shilingi kwa sekunde, ikipandisha bei itangaze au ikikata kinyemela ishitakiwe
6. Waziri asiwe mbunge
7. barabara ikitaka kupita kwenye eneo la makazi ya watu, wasilipwe fidia bali serikali ile gharama stahiki za kununua nyumba eneo lile
8. mwananchi ndio mwenye nchi
Saturday, June 2, 2012
Friday, June 1, 2012
PRICELESS MEMORIES
#ZANZIBAR REVEALED
Hapa panazuka swali; kama lengo la Hamud la kumuua Karume lilikuwa kulipa kisasi, kwa nini tukio hili lilihusisha watu zaidi ya mmoja? Si hivyo tu; kwa nini watu zaidi ya 1,000 walikamatwa kutokana na mauaji hayo kama haukuwa mpango mpana?
Katika kutekeleza mapinduzi hayo, ambayo mipango na operesheni yake ilifanana kabisa na ya mapinduzi ya 1964, mtu mmoja, Suleiman Sisi, alipewa jukumu la kuongoza mashambulizi kwenye Kambi ya Jeshi la Mtoni na Ahmada alipewa jukumu la Kambi ya Bavuai, Makao Makuu ya Jeshi la Chuo cha Jeshi la Mafunzo ya Redio ambazo zote ziko eneo la Migombani.
Kambi ya Ubago haikupangiwa mtekaji kwa kuamini kwamba kama kikosi cha Ahmada kingeweza kuziteka sehemu kilichopangiwa, Ubago ingesalimu amri sawia.
Kituo cha Polisi Malindi kingetekwa na kikosi ambacho kingeongozwa na Hamud, ambapo magari yenye redio za mawasiliano yangepatikana kwa watekaji. Ilipangwa kuwa wakati mashambulizi haya yakiendelea, kituo cha Polisi Ziwani kingevamiwa na askari polisi walitarajiwa kuajiriwa na kuongozwa na askari Yusuf Ramadhan.
Mtu mwingine, Amour Dughesh, alipangwa kuteka Ikulu na alipewa jukumu lakumkamata Karume na kumpeleka Kituo cha Redio kutangaza kupinduliwa kwa Serikali rake.
Inaelezwa pia kwamba baada ya redio kutekwa, ingewekwa chini ya udhibiti wa Badawi Qualletein, Miraji Mpatani na Ali Mtendeni. Uwanja wa Ndege ungedhibitiwa na Ali Sultan Issa, ambapo Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa AS P (ASPYL) yangetekwa na Baramia.
Makao Makuu ya ASPYL yalikuwa Kituo Kikuu cha Mkuu wa Usalama wa Ndani ya Serikali ya Karume, Kanali Seif Bakari. Kanali Bakari aliongoza kikundi cha ukatili kilichojiita kamati ya watu 14, kilichotesa na kuua waliodhaniwa wapinzani na Karume. Abdulrahman Mohammed Babu, akiandikia jarida la kila mwezi 'CHANGE' (Vol 4 No. 7,) la 1996, ukurasa 11, anakiri:- "Kutaja pekee jina la Kamati ya Watu 14 kulitosha kumtia mtu woga na kutishika”.
Kamati hii ilihusika na mauaji ya mamia ya Wazanzibari wasio na hatia, wakiwemo, viongozi, wana’mapinduzi wa kimaendeleo kama Abdallah Kassim Hanga, Abdulaziz Twala, Saleh Saadala, Othman shariff na wengine wale waliuawa kwa jina la Karume."
Abdallah Ameir alipewa jukumu la kuzuia mashambulizi kutoka nje siku hiyo yamapinduzi.
Ukiwaondoa Luteni Hamud na Kepteni Ahmada katika mpango huu, na kama ni kweli kwamba mpango wote ilikuwa jaribio la mapinduzi (coup d'etat) kama ilivyodai Serikali ya Zanzibar, 'basi staili ya mpango huo haiwezi kutofuatishwa na ile ya mapinduzi ya umwagaji damu ya Aprili 12, 1964 ,ambao haukuhusisha jeshi.
Na kama ni kweli ilivyosema Serikali ya Zanzibar, kwamba mpango wa mapinduzi ya 1972 ulibuniwa tangu mwaka 1968, ilikuwaje JWTZ na Usalama wa Taifa, achilia mbali kikosi cha Usalama wa Ndani cha Karume (Gestapo), kilichoongozwa na Kanali Seif Bakari kisibaini mapema hadi siku ya kupoteza uhai wa Kiongozi wa.taifa hilo? Je, si kweli kwamba historia ya 1964 ilikuwa ikijirudia?
Haya yanaweza kuwa maoni ya wengi, wakiwamo wachunguzi wa mambo ya siasa. Mwanazuoni mahiri barani Afrika, Ali Mazrui anabainisha katika kitabu chake 'Africa's International Relations' (uk. 11); "ukizingatia jinsi Sheikh Abeid Karume alivyoitawala Zanzibar kwa ukatili na ubaguzi mkubwa, lolote lilitarajiwa kutokea kwake; hakuna aliyetarajia kwamba angedumu kwa miaka minane madarakani. Ndiyo maana hatimaye wengi hawakushangaa alipouawa mwaka 1972."